Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zichukuliwe kutokomeza kutumikishwa: ILO

Hatua zichukuliwe kutokomeza kutumikishwa: ILO

Ripoti mpya kutoka kwa Shirika la kazi duniani ILO imeangazia hatua zinazostahili kuchukuliwa ili kumaliza ajira za lazima ambapo wanawake , wanaume na watoto milioni 21 kote duniani wanadhulimiwa na kusafirishwa kiharamu kwa biashara ya ngono na utumwa. Kulingana na ILO jitihada za kutambua na kuzuia visa vya ajira  za lazima mara nyingi zimeshindwa kuzaa matunda hata baada ya hatua zilizochukuliwa na baadhi ya nchi . Ripoti hiyo imetolewa na ILO kabla ya kuandaliwa kwa mkutano wa wataalamu kuhusu kazi za lazima wanaowawakilisha serikali , wafanyikzi na waajiri. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(SAUTI ASSUMPTA)