Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima Misri watarajia mabadiliko katika kilimo: ILO

Wakulima Misri watarajia mabadiliko katika kilimo: ILO

Wakati msismko wa mapinduzi ya mwaka 2011 bado unahisiwa nchini Misri, wakulima wengi nchini humo wanatarajia kwamba sekta ya kilimo nayo itafikiwa na mabadiliko mazuri.

Wakulima hao wanatarajia mabadiliko katika sheria, wakisaidiwa na Shirika la Ajira Duniani, ILO, ili biashara zao za kilimo ziwe na faida zaidi.

Inatarajiwa kuwa hali hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi, kwani kilimo kinachangia kwa kiasi kikubwa zaidi mapato ya jumla ya taifa la Misri, hata ingawa ardhi inayoweza kulimwa ni chini ya asilimia 4 ya nchi nzima. Jason Nyakundi na taarifa kamili