Ban akaribisha mazungumzo ya Kachin

7 Februari 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha na kupongeza hatua ya kuwepo kwa mazungumzo yenye shabaha ya kutanzua mkwamo wa eneo la Kachin la China na Mynmar.

Pande zote mbili zimetoa taarifa ya pamoja iliyoelezea namna zilivyodhamiria kuanzisha majadiliano ili kuepusha uwekekano wa kuzidisha machafuko katika jimbo la Kachin linalowaniwa na pande zote mbili.

Akizungumzia hiyo ya pamoja iliyotolewa na pande zote mbili, Ban pamoja na kuzipongeza lakini amezihimiza kuendelea kukaribisha majadiliano ili kupatikana kwa suluhu ya kudumu.

Katika taarifa yake Ban amesema kuwa ni matumaini yake kuona kwamba yale yaliyofikiwa wakati huu yataendelea kulindwa na hatimaye kufikia shabaha ya kutanzua jumla mzozo huo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter