Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadhaniao huduma za posta zinakufa wanaota ndoto ya mchana: UPU

Wadhaniao huduma za posta zinakufa wanaota ndoto ya mchana: UPU

Kadri maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yanavyozidi kuibuka, baadhi ya watu wamekuwa na hofu juu ya hatma ya huduma za posta, wakidhani kuwa matumizi ya barua pepe, simu za mkononi na hata utumaji wa pesa kwa mtandao ni hati ya kifo kwa huduma za posta. Mkurugenzi Mkuu wa muungano wa mashirika ya posta duniani, UPU, Bishar Hussein anasema La hasha! Sasa ndio huduma za posta zinashamiri kwani teknolojia ya mawasiliano mathalani imeibua huduma mbali mbali ikiwemo biashara mtandao. Usafirishaji wa vifurushi kwa posta ndio unashamiri, hivyo basi kudhani kuwa posta inakufa ni sawa na ndoto ya mchana. Ushauri wake mkubwa ni kwamba mashirika ya posta yawe na ubunifu ili yaende na wakati. Bwana Hussein alisema hayo na mengine mengi katika mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja  wa Mataifa. Hapa anaanza kwa kujibu swali kuhusu hatma ya huduma za posta.