Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay alaani mauaji ya mtetezi wa haki za binadamu nchini Tunisia

Pillay alaani mauaji ya mtetezi wa haki za binadamu nchini Tunisia

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amelaani mauaji ya Katibu Mkuu wa kikundi cha vuguvugu la wazalendo nchini Tunisia, DPM, Chakri Belaid.

Pillay amesema amehuzunishwa na taarifa za kifo cha Belaid ambaye alikuwa mtetesi mkubwa wa haki za binadamu na akipinga vurugu za kisiasana kueleza kuwa kifo chake ni pigo kubwa kwa demokrasia nchini Tunisia.

Mtetesi huyo wa haki za binadamu alipigwa risasi alipokuwa akiondoka nyumbani kwake mjini Tunis mapema siku ya Jumatano.

Cécile Pouilly ni afisa wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.