Kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa CAR, Ban asifu

5 Februari 2013

Taarifa za kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati zimepokelewa kwa pongezi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon.

Upande wa serikali na wale wa upinzani wamefikai hatua hiyo kufuatia makubaliano yaliyotiwa saini huko Libreville, Gabon tarehe 11 mwezi uliopita ambapo Bwana Ban amesema hatua hiyo ya hivi karibuni zaidi ni muhimu katika kuimarisha mchakato wa kujenga amani nchini humo.

Katibu Mkuu amekaririwa akiwawatia shime wahusika wa pande zote nchini humo kuheshimu vipengele vya makubaliano hayo na kuchukua hatua muafaka kuhakikisha wanalinda raia nchini kote.

Halikadhalika amesisitiza umuhimu wa Jumuiya ya kimataifa kusaidia haraka mahitaji ya kibinamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati