Mashauriano ya dhati kati ya Palestina na Israeli ndiyo suluhu pekee: Ban

5 Februari 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amefungua kikao cha kamati ya haki za kimsingi za wananchi wa Palestina na kusema kuwa ujenzi wa makazi wa walowezi unaofanywa na Israel kwenye Ukingo wa magharibi wa mto Jordan na Yerusalem Mashariki ni batili.

Amesema ujenzi huo siyo tu ni kinyume na sheria ya kimataifa bali pia ni kikwazo kikubwa kwa suluhisho la mgogoro baina ya pande mbili hizo la kuwa na mataifa mawili.

Bwana Ban pia ametaka hatua zaidi kuchukuliwa ili kushughulikia hofu ya Israeli juu ya usalama wake huko Ukanda wa Gaza, akifafanua kuwa ni muhimu kudhibiti mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo pamoja na kuingiza silaha kimagendo kwenye eneo hilo.

Hata hivyo kubwa zaidi amesisitiza mashauriano ya dhati baina ya Palestina na Israeli ambayo amesema ndiyo yanayoweza kumaliza mzozo huo na kupata suluhisho la mataifa mawili yatayayokuwepo pamoja na kwa amani.

(SAUTI YA BAN)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter