Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera mpya zahitajika kuboresha kilimo cha miti na mimea ya kilimo:FAO

Sera mpya zahitajika kuboresha kilimo cha miti na mimea ya kilimo:FAO

Mamilioni ya watu wanaweza kujikomboa kutoka kwenye umaskini, njaa na kuharibika kwa mazingira ikiwa mataifa yatafanya juhudi zaidi katika mbinu za  kujumuisha kilimo cha miti na mimea ya chakula au na kilimo  cha mifugo.

Hii ni kwa mujibu wa Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO, ambalo limesema kuwa sekta ya kilimo cha miti na mimea ya chakula inaweza kutoa mchango katika kuzalisha mazao tofauti yakiwemo mbao, kuni matunda na chakula cha mifugo ikiwemo pia kahawa na mpira. Taarifa zaidi na Alice Kariuki

(Taarifa ya ALICE KARIUKI)