Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNESCO aanza ziara Tanzania

Mkuu wa UNESCO aanza ziara Tanzania

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Irina Bokova yuko nchiniTanzaniakwa ziara rasmi ya siku tatu ambapo atakuwa na mazungumzo na viongozi mbali mbali.

Taarifa kutoka tovuti ya UNESCO inasema viongozi hao ni pamoja na mawaziri wa Mawasiliano, Sayanasi na Teknolojia, Elimu na Mafunzo ya Ufundi, pamoja na Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Halikadhalika Bokova atakutana na mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchiniTanzaniakabla ya kwendaZanzibar.