Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marathoni kuinua hadhi ya Nairobi kama mji mkuu wa mazingira wa dunia.

Marathoni kuinua hadhi ya Nairobi kama mji mkuu wa mazingira wa dunia.

Baadhi ya wanariadha mashuhuri wa Kenya wa marathoni na wale wanaoibukia watashiriki katika mbio maalum zilizoandaliwa na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP mjini Nairobi kwa lengo la kuinua zaidi hadhi ya mji huo kama mji mkuu wa uhifadhi wa mazingira wa dunia.

UNEP inasema mbio hizo za kilometa 21 zitakazofanyika tarehe 24 mwezi huu zitashirikisha pia wananchi wa kawaida, wanadiplomasia na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Mbio hizo zimeandaliwa na UNEP kwa kushirikiana na taasisi ya Paul Tergat mwanariadha mashuhuri waKenyapamoja na chama cha riadha chaKenyakwa msaada wa kamati ya kimataifa ya olimpiki.

Nick Nuttal ambaye ni Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano ya umma cha UNEP amesema uamuzi wa kuinua hadhi ya shirikahilounaamanisha kuwaNairobikwa sasa ni makao makuu ya mazingira ya dunia.