Watoto DRC watumia sanaa kuelezea madhila yao

4 Februari 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na washirika wake wamewezesha watoto huko Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia yaCongo, DRC ambao walikumbwa na athari za kisaikolojia kutokana na mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi, kuweza kuelezea fikra na madhila yaliyowakumba kupitia sanaa na uchoraji.

UNICEF imetenga eneo maalum la watoto kwenye kambi ya Mugunga III iliyoko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini ambapo watoto wanapata fursa ya kueleza yale waliyoshuhudia wakati wa mapigano kati ya waasi wa M23 na majeshi ya serikali.

Kupitia michoro hiyo watoto wa kike wameweza kuelezea matukio ya kubakwa pamoja na uhalifu mwingine ambao wenzao walitendewa wakati wakifanya kazi zao za kila siku za nyumbani.

Miongoni mwa mashuhuda hao ni mtoto huyu ambaye jinalakelimehifadhiwakwa usalama wake na anaelezea alichokiona kupitia mchoro wake.

(SAUTI  YA MTOTO)

Mtoto mwingine wa kike akaelezea jinsi mwenzao alivyokamatwa wakati akitoka kuokoa kuni.

(SAUTI YA MTOTO)

Eneohilolinawezesha watoto zaidi ya Elfu Tano wa kike na wa kiume kila siku kufika na kuchora kwa lengo la kuelezea fikra zao.