Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani shambulio kwenye Ubalozi wa Marekani nchini Uturuki

Baraza la Usalama lalaani shambulio kwenye Ubalozi wa Marekani nchini Uturuki

Kufuatia shambulio dhidi ya Ubalozi wa Marekani nchini Uturuki siku ya Ijumaa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo hicho na kusema kuwa ni cha kinyama huku wajumbe wake wakituma rambirambi kwa wafiwa.

Taarifa iliyotolewa na baraza hilo imesema linasikitishwa na shambulio hilo mjini Ankara  ambalo limesababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi..

Halikadhalika wajumbe wa baraza wamelaani vitendo vya mara kwa mara vya mashambulizi dhidi ya maafisa wa kibalozi na wawakilishi wa nchi za kigeni ambavyo wamesema siyo tu vinatishia usalama wao bali pia vinasafanya washindwe kufanya kazi zao kwa kawaida.

Baraza limesisitiza umuhimu wa kupiga vita ugaidi kwa mbinu zote kwa mujibu wa katiba iliyoanzisha Umoja wa Mataifa na kusema kuwa vitendo vyovyote vya kigaidi ni uhalifu na haviwezi kuhalalishwa kwa sababu yoyote ile.