1 Februari 2013
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman amewasili nchini Burundi kwa ziara ya siku mbili. Afisa huyo Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na wawakilishi wa vyama vya kisiasa.
Tayari Bwana Feltman amekuwa na mazungumzo hii leo na wawakilshi wa Mashirika ya kiraia.
Ziara yake inanuwia kuelea vema Burundi na kuunga mkono kazi ya Umoja wa Mataifa nchini humo.
Mwandishi wetu mjini Bujumbura Ramadhani KIBUGA anatuarifu zaidi.
RIPOTI YA RAMADHAN KIBUGA