Watoto 210,000 mjini Homs wanahitaji msaada wa kibinadamu: UNICEF

1 Februari 2013

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye mji wa Homs nchini Syria umegundua kuwa jumla ya watu 420,000 nusu yao wakiwa ni watoto wanahitaji msaada wa dharura. Shughuli hiyo ya mwezi mzima ambayo tayari imekamilika iligundua kuwa  karibu watu 700,000 kwenye mji huo waliathiriwa na mzozo ulishuhuhudiwa wakiwemo watu 635,000 waliolazimika kuhama makwao.

Watoto ndio walioathirika zaidi  na kulingana na mtaaalamu wa masuala ya dharura kwenye shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Mark Choonoo ni kuwa watoto wengi walionyesha dalili za dhiki wakitaka msaaada wa kuwatuliza. Msasada wa UNICEF mjiniHomsni pamoja na mablanketi, vifaa vya usafi na nguo za watoto. Kati ya ajenda kuu ni pamoja na kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto, kutoa nafasi za masomo na kuboresha huduma za maji. Hivi majuzi UNICEF ilitoa wito wa dola milioni 68.5 zitakazofadhili programu za kuokoa maisha nchiniSyriakwa kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2013 lakini ni kiwango kidogo tu cha fedha kilichotolewa.