Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya polisi wa kike kwenye Umoja wa Mataifa iongezwe: ORLER

Idadi ya polisi wa kike kwenye Umoja wa Mataifa iongezwe: ORLER

Mshauri mkuu wa masuala ya polisi kwa Umoja wa Mataifa anayemaliza muda wake Ann- Marie Orler ametoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja huo kutuma polisi zaidi wa kike wenye sifa za juu kuhudumu kwenye oparesheni zake.

Orler ambaye mtaalamu wa sheria amesema mwaka 2009 Umoja wa Mataifa ulizindua mpango mahsusi wa kuongeza idadi ya polisi wa kike kwenye huduma za Umoja wa Mataifa hadi asilimia 20 ifikapo mwaka 2014.

Bi Orler amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani kuwa hata kama idadi ya polisi wa kike imeongezeka kwa muda wa miaka mitatu unusu iliyopita kwa sasa ni aslimia 10 tu ya polisi wa kike wanaohudumu kwenye Umoja wa Mataifa.

Ametoa mfano wa Rwanda, ambayo amesema mwezi uliopita ilituma jopo la maafisa polisi wa kike 15 kwenda Cote D’Ivoire. Amesema Rwanda, Bangladesh na India zinaongoza kwa kupeleka maafisa polisi wa kike kuhudumu ndani ya Umoja wa Mataifa