Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lakutana kujadili umuhimu wa uongozi wa kisheria

Baraza la Usalama lakutana kujadili umuhimu wa uongozi wa kisheria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili umuhimu wa kuimarisha uongozi wa kisheria kama njia ya kuendeleza amani na usalama wa kimataifa.

Akilihutubia Baraza hilo wakati wa kufungua mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, amesema kuhakikisha haki na usalama kupitia uongozi wa kisheria ni njia mwafaka ya kuepuka migogoro na kupunguza hatari ya kutumbukia tena katika mizozo.

Bwana Eliasson, ambaye amelieleza Baraza hilo kuhusu kile ambacho Umoja wa Mataifa unafanya ili kuhakikisha uongozi wa kisheria unanawiri, amesema juhudi za UM zinazingatia njia za kina zinazohusisha haki, usalama na maendeleo, kwa lengo la kuyafikia makundi ya watu ambao wamo hatarini zaidi.

(SAUTI YA ELIASSON)