Athari za kimbunga Msumbiji, mama ajifungulia juu ya paa: OCHA

30 Januari 2013

Kimbunga Felling kimezidi kusababisha madhara huko Msumbiji wakati huu inapotolewa hadhari kuwa kinasonga kaskazini ambapo licha ya zaidi ya watu 48 kupoteza maisha na nyumba kuharibiwa za wakazi 250,000, mwanamke mmoja mjamzito amejikuta akijifungulia juu ya paa la nyumba.

Mama huyo aliyetambulika kwa jina la Hortensia ni mkazi wa wilaya ya Chokwe nchini Msumbiji, moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi na mafuriko hayo. Hortensia alijifungua salama mtoto wa Kike akiwa juu ya paa.

(SAUTI YA Hortensia)

Mvua zilipoanza nilipanda kwenye paa la nyumba ya jirani yangu ambapo hatimaye nilijikuta najifungua. Nilikuwa peke yangu lakini baadaye nilipata msaada kwa watu ambao walinishauri niteremke kwa sababu walihofu kuwa ninaweza kupata athari mbaya za uzazi. Baada ya hapo nilipelekwa kwenye makazi ya muda.”

Maafisa wa hali ya hewa wameonya uwezekano wa kutokea mvua kubwa zaidi na wamewataka wakazi kwenye maeneo hayo kuchukua tahadhari.

Nchini Ushelisheli ambako kumetokea mafuriko makubwa pamoja na kusababisha uharibifu wa ardhi kumetangazwa hali ya hatari. George Njogopa ana maelezo zaidi kuhusu hali katika eneo hilo zima.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter