Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ongezeko la wanaouawa na askari wa Israel latia wasiwasi UM

Ongezeko la wanaouawa na askari wa Israel latia wasiwasi UM

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa  James W. Rawley ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuongeza kwa watu wanaouawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel kwenye Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.

Imeripotiwa kuwa tangu mwezi Novemba mwaka jana raia wanane wa kipalestina wakiwemo watoto watatu na mwanamke mmoja wameuawa katika visa tofauti kwenye eneo hilo.

Taarifa imemkariri mratibu huyo akisema kuwa ni lazima kudumishwa kwa haki ya kuandamana kwa amani na kuweza kujizuia ili visa vya mauaji visitokee. Ametaka visa hivyo vya matumizi ya nguvu kupita kiasi vichunguzwe kwa njia huru na wahusika wafikishwe mbele ya sheria.