Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumieni mkutano kuonyesha mnawajali raia wa Syria: Amos

Tumieni mkutano kuonyesha mnawajali raia wa Syria: Amos

Mkuu wa shirika la uratibu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, Valerie Amos amewasihi washiriki wa mkutao wa wahisani kwa ajili ya Syria huko Kuwait kutumia fursa ya mkutano huo kuonyesha kuwa wanajali na kushirikiana kuwasaidia wananchi wa Syria.

Bi. Amos amesema mahitaji nchini Syria ni makubwa. Ametoa mfano kuwa nusu ya hospitai za umma zimeharibiwa, theluthi moja ya zilizobakia hazifanyi kazi, kuna uhaba wa dawa, vyakula na hata kupata tiba ni changamoto.

Amesema fedha zitakazopatikana zitatumika katika maeneo manne ambayo ni ununuzi wa vifaa vya misaada, usaidizi kwa wakimbizi wa ndani na nje ya Syria, ujenzi wa miundombinu muhimu na kuwasaidia mafukara wasitumbukie kwenye maisha ya dhiki zaidi.