Utata uliopandikizwa kwenye tamko la Geneva juu ya Syria uondolewe: Brahimi

30 Januari 2013

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu kuhusu mgogoro wa Syria, Lakhdar Brahimi amelieza Baraza la Usalama kuwa hali ya Syria ni mbaya na kwamba anaona aibu vile ambavyo kila wakati amekuwa akirejea kauli hiyo bila hatua dhahiri kuchukuliwa.

Bwana Brahimi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kulipata baraza hilo taarifa kuhusu hali halisi ya Syria na mazungumzo yanayoendelea ya kutatua mzozo huo.

Amesema mauaji yanaendelea, hali ya kibinadamu ni mbaya hali ambayo amesema baraza imeitambua na kwamba amelitaka lichukue hatua kuhakikisha tamko la Geneva kuhusu Syria linatekelezwa haraka.

Hata hivyo amesema tamko hilo kama lilivyo lenyewe haliwezi kutekelezeka bila Baraza la Usalama kuchukua hatua kwa kuwa kuna kile kinachoonekana kuwa ni utata juu ya mamlaka ya chombo cha mpito Syria.

(SAUTI BRAHIMI)

Bwana Brahimi amesema baadaye usiku huu atakuwa na mlo maalum na wawakilishi wa nchi tano zenye ujumbe wa kudumu katika baraza la usalama ambapo watajadili jinsi ya kuondoa utata huo wa mamlaka ya chombo cha mpito.

Alipoulizwa iwapo yuko tayari kujiuzulu kutokana na kile kinachoendelea Syrai na suluhu kutopatikana, Bwana Brahimi amesema.

(SAUTI YA BRAHIMI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter