Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaimarisha usaidizi wake kwa watoto huko CAR

UNICEF yaimarisha usaidizi wake kwa watoto huko CAR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linaimarisha operesheni zake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kusaidia maelfu ya watoto wanaohitaji misaada ya dharura baada ya kujikuta katikati ya mzozo unaoendelea hivi sasa nchini humo.

Mwakilishi wa UNICEF nchini huko Souleyman Diabate amesema wamebaini maeneo ambako watoto wameathirika zaidi ni pamoja na N’dele, Bria, Bombari, and Kaga ambako watoto wanaishi katika mazingira magumu kupindukia.

Katika taarifa amekaririwa akisema kuwa ni vyema sana kuwafikia watoto hao hivi sasa na kuwapatia misaada lakini wametaka pande zote husika kuweka ustawi wa kudumu wa watoto hao kama kipaumbele na muhimu sana katika kupatia suluhu mgogoro huo.

UNICEF inasema mzozo wa sasa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati umeathiri watu karibu Milioni Moja nukta Nane ambapo Laki nane wanahitaji misaada ya dharura.

Misaada ya haraka inayohitajika ni pamoja na chakula, dawa, maji safi na salama, elimu na ulinzi na kwamba dola Milioni Mbili nukta Moja zahitajika mara moja kusaidia shughuli hiyo..