Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali nchini Libya bado si nzuri: Mitri

Hali nchini Libya bado si nzuri: Mitri

Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Tarek Mitri amelihutubia Baraza la Usalama hii leo mjini New York, Marekani na kueleza kuwa hali ya usalama nchini Libya bado ni mbaya na jitihada za kuimarisha usalama zinaendelea.

Bwana Mitri amesema licha ya kuwepo kwa maendeleo thabiti katika baadhi ya sekta ikiwemo kurejesha ujirani mwema na maheshimiano na nchi jirani na jumuiya ya kimataifa bado hali ya usalama si shwari.

(SAUTI YA MITRI)