Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaonya uwezekano wa kutokea tena homa ya mafua ya ndege

FAO yaonya uwezekano wa kutokea tena homa ya mafua ya ndege

Shirika la chakula na kilimo FAO limeonya juu ya kitisho cha kuzuka tena ugonjwa wa mafua ya ndege ulioikumba dunia mwaka 2006 na limetaka kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kudhibiti kutojirejea kwa hali hiyo.

FAO imesema kuwa wakati dunia ikiendelea kuhangaika na mikwamo ya kiuchumi, kuna kiasi kidogo cha fedha kinachotengwa kwa ajili ya kushughulikia kutojitokeza tena kwa virusi aina ya H5N1 waliosababisha kusambaa kwa ugonjwa huo.

Afisa wa ngazi za juu wa FAO Juan Lubroth amesema kuwa anashangazwa na mwenendo wa dunia kuhusiana na uchukuaji hatua wa kujikinga dhidi ya virusi hao ambao walisababisha hasara kubwa kwa baadhi ya mataifa.

Amesema hali ya wasiwasi imeanza kujitokeza katika baadhi ya mataifa ikiwemo katika nchi za Asia, na katika eneo ka Mashariki ya kati hivyo amehimiza udharura wa kuchukua hatua za kukabiliana na kitisho hicho.