Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yarejesha huduma za usambazaji wa chakula mjini Kismayo

WFP yarejesha huduma za usambazaji wa chakula mjini Kismayo

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza tena usambazaji wa msaada wa chakula kwenye mji wa Kismayo ulio kusini mwa Somalia ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka minne iliyopita.

Mizozo pamoja na ukosefu wa usalama vimekuwa vikiizuia WFP na mashirika kadhaa ya kutoa misaada ya kibinadamu kufanya kazi katika eneo hilo lakini baada ya kuimarishwa kwa usalama sasa ni rahisi kuwafikia watu wanaotaabika mjini humo. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)