Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asifu waliojitolea kuwaokoa wahanga wa mauaji ya kimbari ya wayahudi

Ban asifu waliojitolea kuwaokoa wahanga wa mauaji ya kimbari ya wayahudi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon amesema siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya waliokufa kwenye mauaji ya kimbari ya kiyahudi inatoa fursa ya kutambua mchango wa wale waliojitolea uhai wao kuokoa wahanga wa mauaji hayo licha ya mazingira magumu.

Bwana Ban amesema hayo kwenye ujumbe wake alioutoa kwa njia ya video wakati wa kumbukumbu hiyo mjini New York Marekani iliyokuwa na maudhui Uokozi wakati wa mauaji ya kimbari ya wayahudi: Ujasiri wa kujali.

Amesema mipango ya Adolf Hitler ya kuwaweka kwenye kambi za mateso na kuwaua watu waliokwenda kinyume na imani yake haikufanikiwa kwa sababu baadhi yao waliweza kukimbia kutokana na ujasiri wa wanawake na wanaume waliokuwa tayari kwa lolote ili kuwaokoa wengine.

(AUDIO-BAN)

Hata hivyo baadhi yao waliweza kuepuka kuchinjwa. Waliepuka hiyo kwa sababu ya watu wachache jasiri ambao waliweka hatarini maisha yao na hata familia zao ili kuokoa familia za kiyahudi na wahanga wengine waliokuwa wauawe. Baadhi ya waliwapatia hifadhi wahanga hao kwenye makazi yao, na wengine waliwasaidia kuweza kutoroka salama. Baadhi ya simulizi za waokoaji zimepata umaarufu wa kipekee. Lakini nyingi zinafahamika tu kwa wale ambao uhai wao uliokolewa.