Burundi yaitikia wito wa kutokomeza Surua

25 Januari 2013

Shirika la afya duniani, WHO mapema mwezi huu lilitangaza kupungua kwa idadi ya vifo vitokanavyo na Surua kwa asilimia 71 kati ya mwaka 2000 na 2011 duniani, lakini ugonjwa huo bado ni tishio katika baadhi ya maeneo. WHO ilipendekeza kila mtoto apate vipimo viwili vya chanjo dhidi ya Surua ambapo imesema Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wasio na chanjo dhidi ya Surua.

Burundi ni nchi jirani na DRC na kwa kutambua hofu ya surua kuwa tishio wiki hii imeanzisha kampeni ya chanjo ya ziada kwa watoto dhidi ya maradhi ya Surua. Kampeni hiyo inayodhaminiwa na Masharika ya Umoja wa Mataifa ya UNICEF na WHO inanuwia kuhakikisha kuwa ugonjwa huo wa Surua unatokomezwa moja kwa moja kabla ya mwaka wa 2020.

Barani Afrika ni nchi 4 pekee zilizopata chanjo hiyo ya ziada dhidi ya Surua ikiwa ni pamoja na Ghana, Botswana, Sao Tome na Principe pamoja na Burundi. Kutaka kujua jinsi shughuli hiyo ilivofanyika Burundi, jiunge na Mwandishi wetu Ramadhani KIBUGA katika makala haya.

(PKG YA RAMADHAN KIBUGA)