Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatiwa wasiwasi na visa vya utekaji nyara mashariki mwa Sudan

UNHCR yatiwa wasiwasi na visa vya utekaji nyara mashariki mwa Sudan

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa kumeripotiwa ongezeko kwa visa vya utekaji nyara na kutoweka kwa watu hasa wakimbizi kutoka Eritrea miongoni mwa makabila yaliyo eneo la mpaka mashariki mwa Sudan visa ambavyo vinashuhudiwa ndani ya kambi ya wakimbizi.

UNHCR inasemna kuwa kwa muda wa miaka miwili iliyopita wameshuhudi watu wakitoweka kutoka kwa kambi za Shagarab, wengine wakitekwa nyara huku wengine wakisafirishwa kwenda sehemu zingine. Wale wanaotekwa nyara mara nyingi wanashikilia kwa fidia au huwa wanasafirishwa kwa minajili ya ndoa za lazima, dhuluma za kingono au kwa kazi za lazima. Mingoni mwa visa vya hivi majuzi ni utekaji wa wanawake wanne wakimbizi kwenye kambi ya Shagarab uliofanyika tarehe 22 mwezi huu. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

"UNHCR inashirikiana na utawala wa Sudan, ofisi ya kimataifa ya uhamiaji na mashirika ya kibinadamu kupunguza hatari ya utekaji nyara katika eneo hilo. UNHCR pia inasaidia wakimbizi kwenye kambi ya Shagarab katika kuweka mfumo wa kijamii ili kupunguza hatari za usalama."