Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa ombi la msaada kwa wakimbizi nchini Mali

UNHCR yatoa ombi la msaada kwa wakimbizi nchini Mali

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kwa mara nyingine limetoa ombi la msaada wa kimataifa wa kuwasaidia maelfu ya watu ambao wamelazimika kuhama makwao kutoka ma mapigano yanayoendelea nchini Mali.

Tangu kuanza kwa mapigano kaskazini mwa Mali mwaka mmoja uliopita, zaidi ya wakimbizi 150,000 wamekimbilia mataifa jirani yakiwemo Mauritania, Niger na Burkina Faso huku wengine takriban 230,000 wakitafuta usalama ndani mwa Mali. UNHCR inasema kuwa kuna makubalino kati ya mshirika ya kutoa huduma za kibinadamu yaliyo nchini Mali kuwa hali ya kibinadamu kwa sasa nchini Mali inazidi kuwa mbaya.

Mwaka uliopita UNHCR ilitoa ombi la dola milioni 123.7 kwa oparesheni zake nchini Mali lakini hata hivyo ilipokea asilimia 60 ya fedha hizo. Kati ya mahitaji yanayotakikana kwa sasa ni pamoja na chakula , makao , maji safi , afya na elimu.