Burundi yahitaji msaada zaidi kuimarika: UM

25 Januari 2013

Taifa la Burundi linaendelea kupiga hatua katika kuimarisha uongozi na kujikwamua tena kufuatia mizozo ya mara kwa mara, lakini bado linahitaji msaada kutoka jamii ya kimataifa ili kukabiliana na hali tete kisiasa na umaskini. Haya yamesemwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Parfait Onanga-Anyanga, akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Bwana Anyanga amesema kulikwamua taifa kutoka umaskini na kuponya vidonda vya ghasia za muda mrefu ni changamoto kubwa. Ameongeza kuwa wakati taifa la Burundi likijiandaa kufanya uchaguzi, usaidizi wa kimataifa wa kina kisiasa unahitajika ili kupata suluhu kwa mkwamo wa miaka miwili baada ya vyama vya upinzani kususia kushiriki katika uchaguzi wa mwaka 2010. George Njogopa na taarifa kamili

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)