Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga

Ban akutana na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mashauriano na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, wakati wa mkutano wa kimataifa kuhusu uchumi huko Davos, Uswisi.

Bwana Ban na Bwana Odinga wamezungumza kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Kenya ujao mwaka huu, pamoja na haja ya kuhakikisha uchaguzi huru na wa amani nchini humo.

Katibu Mkuu amemshukuru Bwana Raila kwa mchango muhimu wa Kenya kwa vikosi vya Muungano wa Afrika Somalia, AMISOM, pamoja na kuishukuru Kenya kwa ukarimu wa uwenyeji wake kwa wakimbizi. Pamoja na hayo, wamezungumza pia kuhusu nishati endelevu.