Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yazindua ukusanyaji maoni kupitia mtandao wa Intaneti

UNAIDS yazindua ukusanyaji maoni kupitia mtandao wa Intaneti

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na UKIMWI, UNAIDS, limefungua ukurasa huru wa mawasiliano ya kimtandao kwa shabaha ya kukusanya maoni toka pande zote za dunia, mawazo ambayo yatatumika kuratibu njia mpya za kukabiliana na tatizo la UKIMWI duniani.

Zoezi hili la kukusanya maoni kwenye intaneti litaendeshwa kwa muda wa wiki mbili, na kukamilika mnamo Februari 3.

Ufunguzi huu unakuja wakati jumuiya za kimataifa zimeanzisha majadiliano kuhusiana na mpango utakaofuata wa maendeleo. Mpango huu ni ule unaoandaa njia baada ya kukamilika kwa mpango wa sasa wa maendeleo ya melenia ulipangwa kukamilika ifikapo mwaka 2015. Monica Morara na taarifa kamili.

(TAARIFA YA MONICA MORARA)