Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya fidia ya UM yatoa dola bilioni 1.3 kwa taifa la Kuwait

Tume ya fidia ya UM yatoa dola bilioni 1.3 kwa taifa la Kuwait

Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya fidia imewasilisha jumla ya dola bilioni 1.3 kwa serikali ya Kuwait. Fedha hizo ambazo ni deni zinafikisha jumla ya dola bilioni 40.1 ambazo zimelipwa na tume hiyo zikiwa ni kati ya dola bilioni 52.4 zilizolipwa kwa zaidi ya serikali 100 na mshirika ya kimataifa na ambazo zinataolewa kwa karibu wadai milioni 1.5, zikiwa sasa zimesalia dola milioni 12.3 za kulipwa. Taarifa kamili na Jason Nyakundi.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)