Pillay alaani kufungwa kwa Mhariri Thailand

23 Januari 2013

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Binadamu Navy Pillay amelaani vikali hukumu iliyotolewa kwa mhariri na mwanaharakati wa haki za binadamu Somyot Pruksakasemsuk nchini Thailand, akisema kuwa hukumu hiyo ni ya kuudhi, katili na inakwaza juhudi za utetezi wa haki za binadamu katika nchi hiyo.

Mamlaka ya Thailand imemhukumu mhariri huyo kwa kile kilichoelezwa hatua yake ya kuchapisha matoleo kadhaa katika jarida na hatua yake ya kuwa mstari wa mbele kutetea haki za binadamu.

Vyombo vya dola vimesema kuwa machapisho yake hayo yalikuwa ni tishio kwa utawala wa kiimla na yalikwenda kinyume na misingi ya utawala wa kifalme na hekeya zake.

Kulingana na sheria ya makosa ya jinai kipengele nambari 112, mtu anaayekejeli utawala anaweza kuhukumiwa kifungo cha kati ya miaka mitatu hadi kumi na mitano. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter