Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji wa kimataifa kupanda 2013 na 2014: UNCTAD

Uwekezaji wa kimataifa kupanda 2013 na 2014: UNCTAD

Uwekazaji wa kimataifa wa moja kwa moja ulishuka kwa asilimia 18 mwaka 2012 sawia na kiwango kilichoshuhudiwa mwaka 2009 hali ambayo inachangiawa zaidi kutokana na kutokuwepo uhakika miongoni mwa wawekezaji. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD.

Hata hivyo uwekezaji wa kimataifa unatarajiwa kuongezeka mwaka huu wa 2013 na 2014. Utafiti huu unaangazia zaidi uwekezaji wa kimataifa kwenye nchi zilizostawi na zile zinazoendelea , maeneo yanayokua kiuchumi na nchi kunakofanya uwekezaji huo. Kwa kina zaidi utafiti huu utaangaziwa kwenye ripoti ya kimataifa ya mwaka 2013 ambayo itachapishwa mwezi Julai mwaka huu.