Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaomba dola Milioni 303 kwa mwaka 2013

IOM yaomba dola Milioni 303 kwa mwaka 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Uhamiaji IOM limetangaza mahitaji ya dola za kimarekani Milioni 303 kwa ajili ya kugharimia miradi ya misaada ya kibinadamu kwa kipindi cha mwaka huu 2013.

Miradi hiyo usamaria wema iliyopangwa kutekelezwa na IOM miongoni mwake ni ile iliyoanzishwa mwaka uliopita wa 2012 na inatekelezwa katika nchi 16 ikiwemo Kenya, Sudan Kusini, Chad, na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)