Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madhila yanayowakumba wakimbizi wa Syria yaongezeka: OCHA

Madhila yanayowakumba wakimbizi wa Syria yaongezeka: OCHA

Ziara ya siku nne ya ujumbe wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA huko Syria imeibua madhila zaidi yanayowakumba wakimbizi ikiwemo kukosa huduma za msingi kama vile afya, chakula na elimu kwa watoto.

Msemaji wa OCHA Jens Laerke amesema ujumbe huo ukimjumuisha pia Mkuu wa OCHA John Ging, uliweza kutembelea maeneo ya Talbiseh na Homs ambapo ulishtushwa na vile ambavyo watoto wameathirika pia kisaikolojia kutokana na mambo waliyoshuhudia katika mzozo huo unaoendelea nchini humo.

(SAUTI YA JENS LEARKE)