Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lapitisha azimio kuimarisha ulinzi wa amani

Baraza la Usalama lapitisha azimio kuimarisha ulinzi wa amani

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio ambalo kwalo operesheni za ulinzi wa amani zitaweka msingi wa amani ya kudumu kwenye mataifa ambayo yanakumbwa na mizozo.

Azimio hilo namba 2086 lilipitishwa baada ya mjadala wa siku nzima ambapo linaeleza kuwa shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa zinastahili kuendeshwa kwa njia ambayo itadumisha amani baada ya mizozo na kuepusha kujirudia tena kwa mizozo hiyo.

Azimio hilo pia linasisitiza kuwepo kwa wafanyikazi walio na ujuzi na pia kuwepo kwa ushirikiano wa kimataifa , kimaeneo pamoja na mashirika yasiyokuwa ya serikali.