Ban akaribisha hatua ya Myanmar ya kusitisha mapigano kwenye jimbo la Kachin

21 Januari 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tangazo la hivi majuzi la serikali ya Mynamar la kusitisha mapigano kwenye jimbo lililo kakazini la Kachin. Kupitia msemaji wake Ban ametoa wito kwa pande zote kufanya juhudi za kuleta utulivu kwenye jimbo la Kachin hasa kupitia mazungumzo.

Ban pia ametoa wito wa kutolewa nafasi ya kufikiwa kwa watu wanaotaabika ili kurusu kupelekwa kwa misaada na huduma za kibinadamu kwa wanaoihitaji. Utawala nchini Myanmar ulitangaza kusitisha mapigano ya wiki tatu dhidi ya waasi jimbo la Kachim ambapo watu 75,000 wamekimbia makwao tangu kuanza kwa mapigano hayo mwezi Juni mwaka 2011 katika ya vikosi vya serikali na waasi. Akifanya ziara ya siku nne nchini Maynmar mshauri wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Myanmar Vijay Nambiar ametoa wito kwa pande husika kusitisha mapigano na kurejelea mashauriano.