Changamoto za kiafya ni nyingi, lakini zinaweza kukabiliwa: WHO

21 Januari 2013

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Bi Margaret Chan, amesema kuwa nia ya kuondoa machungu kwa mwanadamu ni thabiti, lakini makali yake huathiriwa na uhaba wa rasilmali, uwezo mdogo na misaada mingi isokuwa na utaratibu mzuri.

Akihutubia kikao cha 132 cha halmashauri kuu ya WHO, Bi Chan amesema shirika hilo linahudumu katika mazingira yenye changamoto nyingi, zikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, ukuaji wa idadi ya watu na ongezeko la watu wazee, kuongezeka magonjwa yasiyo ya kuambukiza huku bajeti za sekta ya afya ya umma zikibanwa.

Amewahimiza wanachama wa halmashauri hiyo kujadili njia bora za kuhusisha afya kwenye ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Kikao cha halmashauri hiyo kitajadili mabadiliko katika WHO, magonjwa yaso ya kuambukiza, kuendeleza afya, kujiandaa na kuitikia magonjwa ya kuambukiza, pamoja na mifumo ya afya.

(SAUTI YA M CHAN)