Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la nyuklia Iran, IAEA yazuiwa kuingia Parchin

Suala la nyuklia Iran, IAEA yazuiwa kuingia Parchin

Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA limesema mazungumzo ya siku mbili kati yake na serikali ya Iran kuhusu mpango wa nyuklia wan chi hiyo hayakuweza kumaliza tofauti kati ya pande mbili hizo.

Naibu mkurugenzi Mkuu wa IAEA kuhusu mipango ya ulinzi salama Herman Nackaerts amesema mazungumzo yaliyofanyika Tehran yalikuwa ya kina lakini hayakuwezesha kuhitimisha hoja ya kuoanisha mpango wa nyuklia wa Iran na matumizi ya kijeshi.

Halikadhalika Bwana Nackaerts amesema hawakuruhusiwa kutembelea kituo cha kijeshi cha Parchin.

Hata hivyo amesema pande mbili hizo zimekubaliana kukutana tena tarehe 12 mwezi ujao.