Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wakimbizi wa Syria wanaoingia Jordan yaongezeka

Idadi ya wakimbizi wa Syria wanaoingia Jordan yaongezeka

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa hali ya wakimbizi wa Syria inazidi kuwa mbaya ambapo idadi yao wanaowasili Jordan kwa muda siku imeongezeka maradufu.

UNHCR imesema kwa sasa inapokea wakimbizi 730 kwa siku tofauti na awali ambapo ilikuwa takriban wakimbizi 500 kwa siku wanaingia Jordan.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ndilo lenye jukumu la kupokea wakimbizi hao maeneo ya mpakani na kuwakabidhi kwa UNHCR. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE)