Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jitihada za Burundi kutokomeza umaskini zatiwa shime

Jitihada za Burundi kutokomeza umaskini zatiwa shime

Umoja wa Mataifa umeitolea Burundi msaada wa milioni 600 za dola katika mpango wa nchi hiyo wa kupambana dhidi ya umasikini baada ya taifa hilo kukumbwa na vita vya zaidi ya muongo mzima.

Mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Mataifa ya kudumisha amani Burundi Balozi Paul SEGER amepongeza hatua iliopigwa na nchi hiyo akiwa katika ziara nchini humo pamoja na maafisa wa benki kuu ya dunia.Maafisa hao wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wanafanya makadirio ya hali ilivo kwa jumla nchini Burundi baada ya kukutana na wakuu wa nchi. Taarifa kamili na Muandishi wetu wa Bujumbura Ramadhani KIBUGA.

(PKG YA RAMADHAN KIBUGA)