Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR kupeleka wahudumu zaidi Mali

UNHCR kupeleka wahudumu zaidi Mali

Huku operesheni za kijeshi zikiendelea kaskazini mwa Mali Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linaongeza wafanyakazi wake katika eneo hilo kuwasaidia wale waliokimbia makwao.

UNHCR inasema kuwa tangu Alhamisi idadi ya wale wanaohama makwao imekuwa ikiongezeka wakati raia 2,744 wakiwa wamewasili kwenye nchi jirani tangu kuanza kwa mapigano na mashambulizi ya angani mnamo tarehe 10 mwezi huu.

Wakimbizi wanaripotiwa kuwawasili nchini Burkina Faso wakitumia usafiri wa umma kwa gharama ya juu. Wengi kati ya wanoawasili wanaripotiwa kuwa wanawake na watoto kutoka kabila la Tuareg. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI MELISSA)

Wakati huo huo shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema litarejea operesheni zake za kusambaza chakula cha msaada kaskazini mwa Mali pindi hali ya usalama itakaporuhusu.