Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2013 ni muhimu sana kwa Cote d’Ivoire: UNOCI

Mwaka 2013 ni muhimu sana kwa Cote d’Ivoire: UNOCI

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Cote D’Ivoire, UNOCI Bert Koenders amesema nchi hiyo inahitaji usaidizi kutoka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Akihutubia baraza hilo Bwana Koenders amesema kuwa serikali ya Cote D’Ivoire itahitaji ushirikiano wakati inapojindaa kutatua masuala yaliyopo yakiwemo umiliki wa ardhi na utambulisho.

(SAUTI YA BERT KOENDERS)

Mwaka 2013 utakuwa mwaka mgumu kwa Ivory Cost na kwa UNOCI. Itahitaji usaidizi kutoka kwa baraza lenu. Kufuatia jinsi hali ya usalama ilivyo, udhabiti na mafanikio ya kiuchumi ya Ivory Cost ni muhimu zaidi kwa udhabiti wa Magharibi mwa Afrika.