Israel yajiunga na makataba wa kuzuia uchafuzi wa mazingira

17 Januari 2013

Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu uchumi kwa bara Ulaya UNECE imekaribisha hatua ya Isreal ya kujiunga kwenye mkataba wa uchafuzi wa mazingira na habari kwa umma pamoja na kushirikishwa kwa umma katika utoaji wa maamuzi likiwa ndilo taifa nambari 32 kujiunga na mkataba huo. Mkataba huo ndio wa kwanza wa kimataifa kuhusu uchafuzi wa mazingira unaolenga kuuhakikishia umma habari kuhusu uchafuzi wa mazingira.

Hii ina maana kuwa makampuni yatahitajika kutoa ripoti za kila mwaka kuhusu vichafuzi vya mazingira na hatua ambayo inatarajiwa kuchukuliwa kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuwepo kwa uchumi usioathiri mazingira. Mkataba huo ulibuniwa mjini Aarhus nchini Denmark mwezi juni mwaka 1998 na kutiwa sahihi na nchi za Ulaya na nchi zingine 39 kutoka eneo hilo na kuanza kutumika mwaka 2001.