Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upanuzi wa kilimo huongeza upotevu wa bayonuai: UNEP

Upanuzi wa kilimo huongeza upotevu wa bayonuai: UNEP

Ripoti moja iliyoangazia ukuaji wa shughuli kilimo pamoja uhifadhi wa mazingira katika nchi za Ki-tropiki, imebainisha namna nchi zinavyopata msukumo wa kuendeleza ardhi kwa ajili ya kupata mavuno zaidi.

Ripoti hiyo imesema kuwa, mataifa mengi yanajiingiza katika kile alichokiita maamuzi ya haraka ya kuendeleza ardhi kwa ajili ya kujipatia faida kwenye mazao kama mahindi na mbunga.

Utafiti wa ripoti hiyo imeonya juu ya dunia kushindwa kufikia malengo yanayojulikana kama Anuai ya Aicha, iwapo mwenendo huo matumizi ovyo ya ardhi utaachwa uendelee.

Wataalamu kwenye utafiti huo wamesema kuwa mataifa yaliyoko kwenye ukanda wa Ki-tropiki yameongeza kasi ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo huko nchi Nigeria, Indonesia, Ethiopia, Sudan na Brazil zikiongoza.