Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya ukata UNHCR yajiandaa na ongezeko la wakimbizi Mali

Licha ya ukata UNHCR yajiandaa na ongezeko la wakimbizi Mali

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema licha ya ukata unaolikabili limejiandaa kuwahudumia wakimbizi ambao idadi yao inaweza kuongezeka kutokana na kuendelea kwa mapigano huko Kaskazini mwa Mali.

Wakimbizi hao wanaongezeka ndani ya Mali na hata wengine wanakimbilia nchi jirani za Niger, Burkina Faso na Mauritania ambapo mwakilishi wa UNHCR nchini Niger Karl Steinacker amesema mipango iko tayari na vipaumbele ni kuhakikisha watu hao wanapata maji safi na salama, elimu, ulinzi kwa watoto na kuwaepusha na ukatili wa kijinsia. Monica Morara na maelezo zaidi.

(SAUTI YA MONICA MORARA)