Wasyria kuweni macho mgogoro unararua Taifa: Ban

16 Januari 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewataka wananchi wa Syria kutafakari upya mgogoro unaondelea nchini mwao ambao amesema unazidi kurarua taifa hilo vipande vipande.

Bwana Ban amesema hayo katika taarifa iliyomnukuu kufuatia shambulio dhidi ya Chuo Kikuu Aleppo kwenye mji wa Aleppo nchini Syria ambapo watu zaidi ya 80 wameripotiwa kuuawa na wengi wengi wamejeruhiwa.

Pamoja na kusikitishwa kwake na tukio hilo na kutuma rambirambi kwa familia za wahanga, Bwana Ban amelaani shambulio dhidi ya raia amblo amesema ni kitendo cha kinyama na kutaka pande zote husika kuzingatia sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu.

Ametaka suluhisho la amani dhidi ya mzozo huo, suluhisho ambalo amesema linapaswa kuzingatia matakwa ya demokrasia ya wananchi wa Syria.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter