Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viashiria vya uchumi kudorora vyatoweka: Benki ya Dunia

Viashiria vya uchumi kudorora vyatoweka: Benki ya Dunia

Ripoti ya benki ya dunia ambayo inaangazia hali ya uchumi wa kimataifa imesema kuwa mkwamo mbaya zaidi wa kiuchumi ulioikumba dunia katika kipindi cha miaka mine iliyopita, sasa unaonekana kutoweka.

Ripoti hiyo ambayo imemulika maendeleo ya uchumi wa dunia baada ya mtikisiko wa kiuchumi, imefafanua kuwa, hali iliyosababisha kuyumba kwa uchumi wa dunia haiko tena.

Hata hivyo ripoti hiyo imesema kuwa pamoja na kutoweka kwa hali hiyo lakini hali jumla ya uchumi wa dunia bado iko kwenye kipindi kigumu.

Imesema nchi zenye kipato kikubwa ndizo zinazokabiliwa na wakati mgumu zaidi huku zikishuhudia uchumi wake ukikua kwa kasi ya chini.