G77 na ushawishi wa agenda ya UM: Ban

16 Januari 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kundi la nchi 77 zinazoendelea, G77 pamoja na China zina ushawishi mkubwa wa kusukuma mbele agenda zinazopigamiwa na Umoja wa Mataifa katika miaka ya usoni.

Amesema kuwa wakati Umoja huo wa Mataifa ukiweka vipaumbele ambavyo inakusudia kuvitilia mkazo katika miaka inayokuja ikiwemo mpango wa maendeleo endelevu, pamoja na ujenzi wa dunia yenye mstakabala mwema, G 77 pamoja na China yana nafasi kubwa kusuadia vipaumbele hivyo

Ban aliyasema hayo wakati wa hafla maalumu ya kukabidhi uenyekiti wa kundi la G 77 toka kwa Algeria kwenda kwa Fiji. Tujiunge na Monica Morara kwa taarifa zaidi.

(SAUTI YA MONICA MORARA)